Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokewa kwenye uwanja wa ndege wa Arusha na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman kwa ajili ya Kufunga Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ ) unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC ).  Nyuma ya Mh. Chande ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu akimkaribisha Balozi Seif kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Jioni kwa ajili ya kuufunga Mkutano wa Majaji wanawake Duiniani. Nyuma ya Jaji Makungu ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ta Tanzania Kanda ya Arusha Mh.Stella Mugasha.
 Balozi Seif na Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman wakitoka nje ya uwanja wa ndege wa Arusha kuelekea Hoteli kwa mapumziko kabla ya kuhudhuria Ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Majaji wanawake Duniani hapo Ukumbi wa AICC. Kati kati yao ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Seif Iddi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipokea muhtasari wa Ratiba itakayomkabili wakati wa hafla ya Ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Majaji Wanawake Duniani ( IAWJ ) mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Naura  Spring kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mhamed Chande Othman kushoto yake. Kulia ya Balozi Seif ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha Mh. Stella Mugash.
 Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani { IAWJ } wakiangalia ngoma za Utamaduni waliyoishuhudia wakati wa matembezi yao ya mapumziko ya usiku kwenye kituo cha Utamaduni Mjini Arusha.
 Wajumbe wa Mkutano wa Majaji Wanawake Duniani { IAWJ } unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha { AICC } wakiendelea na  Mkutano wao wa 12 Mjini Arusha. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ na Marry Gwera Afisa Habari wa Mahakama Kuu Dar es salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: