Mwenzeshaji wa Mafunzo ya waandishi wa habari bwana Ndimata Tegambwage akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imedhamini mafunzo ya wapigapicha yatakayofanyika kuanzia kesho katika kituo cha Msimbazi jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na MP5 2011 Entertainment. Pichani katikati ni Afisa mawasiliano na Matukio bi Dangio Kaniki akifatiwa na mratibu wa semina Mpochi Selemani
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imesema itaendelea kuwajengea uwezo wapiga picha za habari kwa kuendela kuwapatia mafunzo ili wapate ujuzi zaidi kwa kuwa wao ni balozi katika kuipasha jamii habari.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Afisa Uhusiano na Matukio wa Kampuni ya Airtel Dangio Kaniki alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa wapiga picha wa habari kuwajengea uwezo kufanya kazi katika mazingira hatarishi.

"Tutaendela kuwapatia mafunzo wapiga picha ili wapate ujuzi zaidi katika utendaji wao wa kazi kwa kuwa mabalozi wetu,na tutawatafutia vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanyia kazi katika mazingira hatarishi" alisema Dangio

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Baraza la Habari (MCT),na kudhaminiwa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya MP5 2011 yanashirikisha wapiga picha kutoka magazeti na TV.

Akizungumza katika mafunzo hayo mshiriki Suleiman Mpochi ambae pia ni mratibu wa mafunzo hayo alisema watanufaika nayo kwa kuwa watajifunza mbinu mpya za kufanya kazi katika mazingira hatarishi pamoja na
kufuata maadili ya taaluma ya waandishi wa habari.

Kampuni hiyo ni mara ya tatu inadhamini mafunzo hayo kwa wapiga picha za habari ambamo Mwezeshaji katika mafunzo hayo Mkongwe wa Habari katika fani ya habari Ndimara Tegambwage aliiomba kampuni kuendela kudhamini mafunzo hayo na kuwapatia zana za kisasa za kazi wapiga picha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: