Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, Dar es Salaam City College (DACICO) Faudhia Hassan,akipiga kura wakati wa zoezi la kuwachagua Viongozi wa Serikali ya wanafunzi kwa nafasi za Rais wa Chuo na Nafasi ya Makamu. Uchaguzi huo umefanyika Makao Makuu ya Chuo, Kibamba Dar es Salaam. (Picha Deogratius Peter).
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, Dar es Salaam City College (DACICO) Rehema Mussa,akipiga kura wakati wa zoezi la kuwachaguaViongozi wa Serikali ya wanafunzi kwa nafasi za Rais wa Chuo na Nafasi ya Makamu. Uchaguzi huo Umefanyika Makao Makuu ya Chuo, Kibamba Dar es Salaam leo.(Picha Deogratius Peter).
---
Na William Severine/Mathias Haule/Grace George (Wanafunzi DACICO).

Wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam City College kilichopo jijini Dar es Salaam leo wamefanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wao katika nafasi ya urais na makamu wa rais kutokana na uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wao.

Wagombea waliojitokeza katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Mathias Canal, Hilary Mgenzi, Christopher Mwakasanga (Urais) na kwa nafasi ya Makamu wa Urais ni pamoja na Razack Mushi, Mathias Haule, na Rozalina Mchomvu.

Aidha mkurugenzi wa chuo Mr. Idrisa Mziray alitoa pongezi kwa wanafunzi wote kwa kujitokeza na kushiriki katika tukio hilo la upigaji kura kutoka na kuwa ni haki yao ya kimsingi ili kujipatia viongozi walio bora kwa maslahi yao na chuo kwa ujumla.

"Uchaguzi Umekwenda Vizuri, kikubwa nawapongeza wanafunzi wote kwanza kwa kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura, pia nawapongeza wasimamizi kwa kuandaa Uchaguzi huru na wa haki maana wametimiza misingi ya Demokrasia, hakuna malalamiko kutoka pande zote, hili ni jambo la kujivunia sana, kwa kuwa chaguzi nyingi vyuoni uambatana na vurugu na pia Rushwa za hapa na pale" alisema Mziray

Matokeo ya Uchaguzi huo yanatazamiwa kutangazwa mapema kesho baada ya kuhesabiwa na wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: