Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa, akimkabidhi Bwana Said Hamad Abdulla mshindi promosheni ya Kwangua na Ushinde zawadi yake ya pikipiki aina ya Vespa katika duka la huduma la wateja la Zantel, Zanzibar.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel imemkabidhi mshindi wa kumi na mbili wa promosheni yake ya Kwangua na Ushinde zawadi ya pikipiki aina ya Vespa.

Mshindi huyo, Bwana Said Hamad Abdulla ambaye ana miaka 36, mkazi wa Unguja, ameishukuru kampuni ya Zantel kwa zawadi hiyo.

‘Naishukuru kampuni ya Zantel kwa zawadi hii ya pikipiki, ambayo kwa hakika itanisaidia katika kurahisisha kazi zangu za kila siku’ alisema Bwana Said.

Promosheni ya Kwangua na Ushinde inawataka wateja wa Zantel, Zanzibar pekee, wapya na wazamani kuingiza muda wa maongezi wa shilingi elfu moja au zaidi ili kushiriki promosheni hiyo.

Mshindi mkubwa wa promosheni hiyo atajinyakulia gari, huku wateja wengine wakijishindia zawadi za kila siku kama muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja, pikipiki aina ya Vespa, komputa ndogo (Huawei Media pads) pamoja na modemu za 3G.

‘Promosheni hii inathibitisha namna kampuni yetu ilivyo msitari wa mbele katika kuboresha maisha ya wateja wetu huku wakiendelea kuwasiliana na ndugu na marafiki zao’ alisema Mohamed Mussa, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel upande Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: