Na Juma Mtanda, Morogoro.

BINGWA wa dunia mkanda wa WBF uzani wa Super Middle, Francis Cheka ‘SMG’ amewaeleza maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika mapokezi yake kuwa ubingwa alioutwaa baada ya kumtwanga bondia Phil Williams wa Marekani kuwa ni ubingwa huo ni wa wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa mapokezi yake katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Olduvai Mafiga Morogoro Cheka alisema kuwa endapo angepigwa katika pambano lake na bondia, Williams aibu ingewaangukia wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla hivyo ubingwa huo ni wa watanzania wote.

 Cheka alisema kuwa yeye ndiye alikuwa mwakilishi kwa Tanzania katika ulingo kupambana na Mmarekani katika kuwania ubingwa wa dunia wa WBF kupitia mchezo wa ngumu na ameshukuru kumkung’uta kama angepoteza pambano hilo ana imani kila mtanzania angejisikia vibaya kutokana na matokeo hayo.
“Nimefurahi kuona watanzania kunipa sapoti katika mchezo huu na nawaomba waendelee hivi hivi kutuunga mkono mabondia wote katika michezo yetu ya kimataifa ili kuweza kufanya vizuri lakini kwa sababu nimemchapa Phil Williams na kutwaa ubingwa huo wa dunia na kubakia Tanzania kuna kila cha kujivunia katika hili”. Alisema Cheka.
Aliongeza kuwa namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa afya njema iliyoniwezesha kunipa nguvu katika pambano lile na kumtwanga mpinzani wangu, sifa hii sio ya Cheka pekee bali ni kwa wana Morogoro na Tanzania kwa ujumla hivyo kila mmoja wetu anayo haki ya kutembee kifua wazi kwa ubingwa huu”. Alisema Cheka.
Cheka alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwake kutokana na aina ya bondia na nchi anayotoka ina mabondia wenye viwango bora duniani hivyo alikuwa makini muda wote wa mchezo kuhakikisha anamtandika makonde mpinzani ili kuweza kumshinda. 

Picha zote kwa hisani ya Juma Mtanda na Dustan Shekidele, Morogoro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: