Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania na kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika.

Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi kombe captain wa timu ya wasichana Tanzania mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika jana jijini Lagos Nigeria.
Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars wakishangilia ushindi
Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika.
Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi wa kikosi cha timu ya wasichana mara baada ya kuibuka washindi katika michuano ya kimataifa ya Airtel Rising stars
TANZANI OYEEEEE!
Kikosi cha timu mabigwa ya Airtel Rising stars Afrika cha wasichana cha Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja pichani waliosimama (wa mwisho kushoto) ni kocha wa timu ya wavulana Abel Mtweve na wa mwisho kulia ni kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage.
---
Timu ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu nchi Nigeria.

Tanzania ilipata ubigwa huo baada ya kuchuana vikali na timu ya Kenya katika mechi ya Fainali na kuifunga Kenya goli moja bila na kuibuka mabingwa . Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania.

Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone , Malawi , na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1 , wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1.

Wakashinda 4-2 katika mikwaju ya penati dhidi ya DRC katika robo fainali mechi zilizopigwa katika uwanja wa NIS Sports. Na wakawatoa Uganda kwa mvua ya magoli 8-1
.
Mbali na ushindi huo wa wasichana watanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface.

Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6 katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.

Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita . Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda.

Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo

Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na Main bowl.

Kulianza na “ gala night” jumapili usiku ikafatia sherehe za ufunguzi , na mechi za ufunguzi za makudi katika uwanja wa AgegeTownship.

Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili , mashindano haya yamekua bora kwa vijana wadogo na kwakuzingatia jinsia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: