Usimbembeleze Mwanaume ambaye umefanya kila jitihada kumpenda na kumpa Mahaba yote na kufanya mambo ambayo ni risk kwa maisha yako na hajali anataka kuondoka... MUACHE AENDE.

Usimlazimishe Mwanamke ambaye umefanya yote kwake,na wakati mwingine kuonekana mjinga ili awe na furaha, umejinyima kutojenga hata kibanda cha uani unaishi nyumba ya kupanga mpaka leo ili umfurahishe kwa Shopping za kila mwezi, Kodi yake ya nyumba, na wengine mmesomesha mademu zenu... Leo kakuona hufai... MUACHE AENDE.

Huwezi kumlazimisha Mwanaume/Mwanamke aliyeamua kwenda abaki wakati hana sababu za wewe kubaki... Hata Mapenzi yana Expiry Date, sio Maziwa Mtindi tu... Chakula kilichochacha hakiwi kitamu kwa kuwekewa Mayonnaise, Tupa jalalani...

Ukilazimishwa utakuwa mtumwa, utaumizwa, na still hatabaki... Kama hajui thamani yako na ameona thamani nyingine nje MUACHE AENDE... Ni wapuuzi tu hung'ang'ania Penzi wakati hawatakiwi, Usiwe mmoja wao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: