Na Mwandishi Wetu

MSANII nguli wa muziki wa dansi aliyestaafu, Muhidini Gurumo, atapanda jukwaani leo kutumbuiza na mkewe, sambamba na kupewa zawadi za heshima.

Gurumo atatoa burudani hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaaga mashabiki, ambapo shughuli hiyo itaambatana na uzinduzi wa kundi la Cash Money, la Tandika mjini Dar es Salaam.

"Tumeandaa zawadi kwa mzee Gurumo kutokana na heshima kubwa aliyonayo katika tasnia ya muziki na kujenga maadili kwa taifa kutokana na nyimbo zake.

Hivyo zawadi zetu zitaenda sambamba na uzinduzi, ambapo tumepanga hivyo, ili lee mwenye chochote ampe mzee wetu,"Aliongeza Latifa Masasi mlezi wa kundi hilo.

Uzinduzi huo unafanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Aziz Ali, Dar es Salaam na utapambwa na bendi mbalimbali za taarabu zikiwemo Coast na G Five.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: