Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel katika wiki ya usalama barabarani, mwandishi huyu alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini na India.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Airtel Tanzania ambao wamekuwa wadhamini wakuu wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa mwaka wa tano mfululizo Bi. Beatrice Singano Mallya akisalimiana na Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Usalama Barabarani nakudhaminiwa na Airtel katika wiki hii ya usalama barabarani mkoani mwanza. Athumani alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini
na India.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi akizungumza ndani ya banda la Zimamoto mara baada ya kutinga mavazi ya kitengo hicho.
Mmoja ya wafanyakazi wa kampuni ya Be Foward akitoa zawadi ya mpira...
------
Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Airtel, Be Forward na Puma kwa kushirikiana wamesema kuwa watahakikisha suala la Usalama barabarani linazingatiwa na jamii ya Watanzania ili kupunguza ajali za barabarani .

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Mallya kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani, yanayofanyika Jijini Mwanza.

Alisema kama wadau wa usalama barabarani,wamedhamini maadhimisho hayo ili kuwezesha jamii kupata elimu na uelewa kuhusu matumizi ya barabara,sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani katika kupunguza ajali nchini.

alisema ajali nyingi nchini zinachelewesha maendeleo na kupunguza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Sisi kama wadau tumedhamini maadhimisho haya kwa mwaka wa tano mfululizo,lengo letu tunataka jamii ipate uelewa na hatimaye kupunguza ajali za barabarani zinaoweza kuepukika,ndiyo sababu tuko hapa,”alisema.

Alisema kutokana na kuonesha umahiri wameanzisha mfumo mpya wa ulipiaji wa leseni za magari kwa kupitia njia ya Airtel Money.

Nae Mkurugenzi mkuu wa Be Forward bw. Daniel Mtaalam alisema.”tunatoa wito kwa watu wote kushirikiana nasi kufanikisha zoezi hili na nimatumaini yetu msaada huu tunaotoa itasaidia katika kupunguza na kudhibiti ajali zinazotokea barabarini nakusababisha maafa makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: