Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw, Gabriel Ondoyo kulia na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakikabidhi Betri za kampuni hiyo kwa  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'EmerGency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kwa ajili ya magari ya kitengo hicho Dar es salaam leo kushoto ni Kaimu Dereva Mkuu Sultan Kitanga na Mkuu wa Idara ya Ufundi ENG,Leonard Elizeus
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kushoto na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakishusha betri walizopeLeka Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kwaajili ya Msaada katika Kitengo Cha Dharura.
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kulia na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakishusha betri walizopeleka Muhimbili kwaajili ya msaada katika kitengo cha Dharura
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kushoto na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya maofisa wa kitengo hicho
Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru Rashidi akikagua betri hizo baada ya kukabidhiwa
Baadhi ya Madereva wa kitengo hicho wakikagua
Baadhi ya wahudumu wakiendelea na shughuli zao katika gari la wagojwa kushoto ni Nikijaeli Ngareni na Josephine Lazaro
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharurua  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kushoto akibadilishana namba za mawasiliano na  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza

Na Mwandishi Wetu

MRATIBU wa Masoko wa Kampuni ya Chloride Exide Bw, Robert Hiza leo ametoa msaada wa Betri mbili katika kitengo cha Emergency Medicine ya hospitali ya Taifa Muhimbili .

Msaada huo wa kwanza kutoa inaendana na miaka 50 ya kampuni hiyo ambapo watatoa viti mbalimbali katika hospital za Serikali vikiwemo Sola kwa ajili ya umeme wa jua . Akipokea msaada huo.Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo amewashukuru kampuni ya Chloride Exide kwa kuliona hilo kwani ni mara ya kwanza katika kitengo chao kupokea msaada kama huo, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali ikiwemo hata magari kama yapo tunaomba msaada maana hapa kitengo chetu ni cha mambo ya dharura na kinategemewa sana kama mnavyojua alisema Prof Victor Mwifongo

Nae  Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru Rashidi amendelea kutoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuliona hilo kwani yeye kama Dereva ameona ni jambo bora sana
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: