Mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya Simu za mkononi ya tiGO, akizungumza na waamiliki wa magazeti tando ‘blog’ (hawapo pichani), waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto)
 Mtangazaji wa kipindi maarufu cha ‘MiniBuzz’ (zamani Daladala), kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star TV kwa sasa, Daniel Kijo, ambaye alikuwa mshereheshaji (MC) wa hafla hiyo ya tiGO, akitangaza utaratibu wa kupata washindi wa bahati nasibu ndogo ya washindi wa ‘moderm’ za tiGO. 
 Mwakilishi wa Kampuni ya simu ya tiGO (kulia), akimkabidhi Henry Mdimu zawadi ya ‘moderm’ aliyoshinda katika bahati nasibu ndogo iliyowahusisha wamiliki wa ‘blog’ katika hafla iliyotayarishwa na tiGO. 
 Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha EATV, Sam Misago (kushoto), akipokea ‘moderm’ aliyoshinda katika bahati nasibu ndogo kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, katika hafla iliyowakutanisha wamiliki na wadau wa magazeti tando ‘blog’ kwenye Hoteli ya New Afrika jana usiku.
Mmiliki wa blog ya Full Shangwe, John Bukuku (kushoto), akipokea zawadi ya  moderm ya tiGO kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni hiyo, baada ya kushinda bahati nasibu ndogo katika hafla hiyo.
 Kocha wa kimataifa wa masumbwi, Rajabu Mhamila ‘Super D’ (kulia), akitania kwa kumkunjia ngumi mmilikiwa blog ya Habari Mseto, Fraancis Dande (katikati), huku Mhariri wa Habari Mseto, Salum Mkandemba akishuhudia.
 Mmiliki wa Habari Mseto Blog, Francis Dande (katikati), akiwa na Mhariri wa blog hiyo Salum Mkandemba (kushoto) na Mpiga Picha wake John Dande katika hafla ya tiGO na wadau wa magazeti tando ‘blog’ kwenye Hoteli ya New Afrika jana usiku.  
 Juu: Washiriki wa shindano la kucheza muziki kwa upande wa wanawake, wakionesha umahiri wao katika kucheza muziki wa Twist, kuwania zawadi ya IPad iliyotolewa na tiGO. Chini: Mshindi akikaabidhiwa IPad hiyo na mmoja wa washiriki wa hafla hiyo.
 Mwanamuziki John Mhina wa Tanzanite, akiimba katika hafla hiyo. 
 Mwanamuziki mkongwe na bloggers, John Kitime akiongea na mmiliki wa blog hii ya Kajunason.
 Hapa burudani inaendelea kama kawaida.
Cathbert Angelo akikabidhiwa Ipad yake baada ya kushinda katika shindano la kucheza muziki kwa wanaume.
 Mmiliki wa blog hii, Cathbert Angelo akifurahia na John Bukuku mmiliki wa Fullshangwe blog (kati) na Josephat Lukaza Mmiliki wa Lukaza Blog.
Mshereheshaji ‘MC’ Daniel Kijo akipozi picha na mmoja wadau walioshiriki hafla hiyo.

Mkurugenzi na Mmiliki wa Blog ya Kajunason Blog, Cathbert Angelo, mwishoni mwa wiki iliyopita alibahatika kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kucheza muziki lililoanadaliwa na Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mikononi ya Tigo Tanzania, katika siku maalum ya kufurahia na wamiliki wa blog mbalimbali katika Hoteli ya New Africa.

Party hiyo ilianza saa moja jioni na kumalizika saa nne za usiku, baada ya kumalizika kwa taratibu mbalimbali zilizoandaliwa na mtandao huo kwa ajili ya kuheshimu na kuthamini mchango wa magazeti tando, yani blog.

Mbali na Angelo, watu mbalimbali katika party hiyo walifanikiwa kujishindia simu, katika tukio hilo lililokutanisha bloggers wengi kwa wakati mmoja na kujadiliana mambo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha kazi zao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: