Afisa uhusiano wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), Bi. Rachel Mkundai akikabidhiwa Tuzo kutoka kwa waandaji “Gender Links”
Afisa Uhusiano wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa tuzo.
Afisa Uhusiano wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), akikabidhi Tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Bw. Peter Maduki.
---
Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) imeshinda Tuzo ya
kutambua mchango wa mashirika ya dini katika kuwawezesha wanawake
kutambua haki ya afya ya uzazi. Tuzo hiyo imetolewa na Shirika
linalotetea masuala ya jinsia (Gender links) ukanda wa nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC) lenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.
CSSC
ilitangazwa mshindi na kukabidhiwa Tuzo hiyo wakati wa kilele cha
mkutano mkuu wa masula ya jinsia ya ukanda huo uliofanyika nchini Afrika
ya Kusini.
Mashindano hayo yalihusisha washiriki 213
kutoka nchi 13 ambazo ni wanachama wa SADC, na CSSC iliibuka mshindi
katika kupengele cha mashirika ya dini na kuwashinda wengine 13 katika
kipengele hicho.
Ushindi wa CSSC umepatikana
baada ya kuwasilisha makala ya filamu (Documentary) kuhusu namna ya
kumsaidia mtoto aliyezaliwa kabla ya miezi tisa (Pre-mature) kukua na
kuongezeka uzito unaostahili kwa kutumia njia ya asili maarufu kama
“Kangaroo method” Njia hii inatumika katika hospitali ya wilaya ya
Sengerema inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Geita
Toa Maoni Yako:
0 comments: