Wanawake na wasichana wa Dar es salaam na mikoa ya jirani Kitchen party gala ipo on tayari.

Mwaka jana ile ya mwisho ya mwezi wa kumi tulifanyia Diamond jubelee VIP hall na ukumbi ulishona sana sana. Kulikuwa na mapungufu kadhaa ambayo sitapenda yajirudie this time. Najua ni mara chache shughuli kukosa upungufu fulani lakini kulirudia kosa ndio kosa zaidi.
Sasa mwaka huu tumepata ukumbi mpya kabisa upo ndani ya jengo la GOLDEN JUBELEE. Hili jengo ni jipya lipo pembeni ya jengo la PPF Tower mjini kabisa. Ukumbi huo unaingiza watu 1000 tu na ndio idadi tunayoitaka siku hiyo.

Service zao ni za kihoteli kabisa na wao ndio wataserve kila kitu. Ukumbi huu uko chini ya JB Belmonte hotel hivyo wao ndio watatoa huduma za chakula. Chakula chetu kitakuwa kwenye hadhi ya starter, main course na desert.

Hivyo tumeona tuadvance ili kukidhi mahitaji yako ya kihuduma, mazungumzo yetu ya siku hiyo na burudani.

Na kwasababu tumeadvance kihuduma na shughuli kwa ujumla kiingilio chetu this time kitapanda kitakuwa Tsh. 40,000/=

Ukumbi una vyoo vingi vipya na visafi na wa hadhi ya kimataifa.Pia najua kina mama ndio waandaaji wa shughuli mbalimbali za kifamilia,marafiki,ukoo mje muone ukumbi huu mpya. Hawa wana kumbi 4 katika jengo hili hili. Unaoingiza watu 1000, 600, 400 na 150 mkuje muone maana tunapata taabu sana ya kumbi hasa kama unataka maeneo ya town.

Tutakuwa na wasemaji wa ndani na nje ya Tanzania. (hapa weka picha ya bendera)

DRESS CODE: Tusisahau dress code yetu ya siku hiyo imekuwa inspired na bendera ya nchi yetu Tanzania.

TAREHE: Kparty Gala itakuwa jumamosi ya tarehe 27 April 2013. Kuanzia saa tano asubuhi mpaka kumi na mbili jioni.

Kwa lolote piga namba hii 0787583132 na 0657442255.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: