Meneja wa PPF Kanda ya ziwa Meshack Bandawe akimkabidhi mifuko ya simenti Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu, mchango wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 2, kwaajili ya kuchangia uharakishwaji wa ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato jijini Mwanza. 

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato Bw. Alfred Wambura, amesema kuwa kamati yake imenuia kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho unakamilika mwishoni mwa mwezi wa 5 na kukabidhiwa kwa jeshi la polisi.

Mikakati mingine iliyowekwa na kamati hiyo ni kukamilisha ujenzi wa nyumba ya makazi ya OSS wa Nyakato pamoja na watendaji wengine watatu wanaomfuata kwa cheo, ili kurahisisha utendaji wa kila siku wa shughuli za usalama wa jeshi hilo. 
Meneja wa PPF Kanda ya ziwa Mesharck Bandawe amesema kuwa ulinzi kwa maisha ya baadaye ya mwananchi uko ndani ya  mfuko wa uwekezaji wa PPF,  na ulinzi wa wananchi na mali zao uko chini ya jeshi la polisi hivyo amewataka wadau wengine wa mashirika mbalimbali kujitokeza kulisaidia jeshi hilo kukamilisha shughuli za utendaji kwa manufaa ya ustawi wa jamii.



Wadau wa PPF wakisikiliza kwa makini yanayojiri kwenye makabidhiano hayo.
Diwani wa kata ya Mahina, Mhe. Chinchibela ametoa rai kwa mashirika mengine kusaidia jeshi la polisi kama sehemu ya ulinzi shirikishi, kwani msaada huu wa PPF umekuwa wa tatu kutoka kwa mashirika mbalimbali mkoani Mwanza ambayo yamethubutu kukisaidia kituo hicho. 
Mhe. Manyerere ambaye ni diwani wa kata ya Nyakato ameishukuru asasi ya PPF kusaidia kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato ambacho ni moja kati ya vituo muhimu kwani kinahudumia usalama wa maeneo ya kata takribani 4 za jiji la Mwanza.
Ujenzi ukiendelea na mchango wa PPF kama unavyoonekana. PICHA/HABARI NA G. SENGO
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: