Rais wa wasafi, Daimond jana Jumamosi aliweza kuudhihirishia umma, kuwa bado anapendwa baada ya kupokelewa kwa shangwe na wakazi wa Manispaa ya Mji wa Bukoba.

Diamond anasema, "Kwanza kabisa ningependa kutanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwa Mwenyezi Mungu kwa siku ya Jana.... (Tarehe 30 Machi 2013) niliwasili salama salimini mjini bukoba Mkoani Kagera.... Pili niwashukuru Mashabiki zangu wote wa mkoani humu kwa mapokezi yao ya hali na mali, hii inaonyesha jinsi gani Watanzania wananithamini na wana mapenzi na wasanii wao..

Anaongeza kwa alilazimaka kutoka juu ya gari kuwasalimu mashabiki wake kabla ya kuelekea hotelini kupumzika na hali ilivyozidi kuwa mbaya polisi walilazimika kufunga barabara kadhaa mjini Bukoba kutokana na umati mkubwa wa watu kuzingira gari alilokuwemo msanii huyo na kila mmoja akitaka kumsalimia. 

Shukrani za dhati; BukobaWadau Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: