Naibu Spika Mhe. Job Ndugai na Mbunge Beatrice Shelukindo wakipokea nishani hiyo kutoka kwa Dkt Mohammed Zaharani (katikati) kwa niaba ya Mama Salma Kikwete. Pembeni wa kwanza ni Bw. Haruna Mbeyu maarufu kama Meya wa London na anayefuatia kabla ya Mhe. Shelukindo ni Bi. Mariam Mungula, Katibu wa Tanzania Women Association (TAWA) UK.
Mhe. Naibu Spika Job Ndugai akipokea Nishani hiyo kutoka kwa Dkt. Mohammed Zaharani. Wakiangalia kwa furaha ni Mhe. Beatrice Shelukindo, Bi Mariam Mungula na Bw. Haruna Mbeyu.
Baadhi ya akina Mama wakitanzania waliohudhuria hafla hiyo katika picha ya upendeleo na Mheshimiwa Beatrice Shelukindo na Nishati ya Mama Salma. Akina Mama wakitamani wote wapande ndege wakaikabidhi Nishani hiyo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwanaharakati wa Kijamii kupitia Chama Chake cha Wanawake na Maendeleleo, wiki iliyopita alizawadiwa Nishani na Chama kinachojishughulisha na kuinua kiwango cha Elimu kwa Nchi za Afrika Mashariki kilichoko katika jiji la London, Uingereza.
Akiongea katika Hafla hiyo fupi iliyofanyikia katika kumbi za Hoteli ya Park Plaza iliyopo pembeni mwa Westminster Bridge (katikati ya jiji la London) Dr Mohammed Zaharan ambae ni Katibu wa Chama hicho cha East Africa Education Foundation (EAEF) alisema kuwa Chama Chake kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu na  shughuli zinazofanywa na Mama Kikwete kupitia Jumuiya ya WAMA na wamefurahi kupata fursa hii ya kumtunukia "Award" kwa mchango wake mkubwa sana wa kuinua Elimu ya Mtoto, hususan wa kike na vilevile kuwezesha Wanawake ili waweze kujitegemea. Dr Zaharani aliongeza kuwa Mama Kikwete ni mfano bora sana wa kuigwa na Wanawake katika jamii ndani na nje ya Tanzania.
Akipokea Nishani hiyo kwa Niaba ya Mama Salma Kikwete, Naibu Spika Mh. Job Ndugai  (Ambae alikuwa Nchini Uingereza kwa Mualiko wa Naibu Spika wa Uingereza na aliongoza na Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utumishi ya Bunge) alisema kuwa amefurahishwa sana na kitendo hicho cha Mchango wa Mama Salma kuonekana, kwa kuwa kinadhihirisha mchango unaofanywa na Jumuiya zisizo za Kiserikali katika jamii kama WAMA unaonekana mpaka Nje ya Tanzania.
Nae Mh. Mama Beatrice Shelukindo alifurahi zaidi kwa kitendo hiki na kusema kuwa hili ni jambo kubwa sana na linadhihirisha mchango mkubwa wa Mama Salma katika kumuendeleza Mwanamke wa KiTanzania na inatoa moyo kwa Wanawake Wengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: