Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,katika kaburi alilozikwa  leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.
 Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi, akiongoza sala wakati wa mazishi ya  Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi, aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya kaskazini B Unguja leo.
 Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
  Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja. 
 
Picha kwa hisani ya Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: