Moja ya miradi iliyoanzishwa mwaka juzi na kampuni ya PSI Tanzania ni usambazaji wa Kondomu katika kumbi za starehe ikiwemo disco na mabaa tofauti yaliyopo katika jiji la Dar es Salam. Tatizo kubwa limekuja ni uendelezaji wa mradi huo ambayo kwa sasa inaonyesha mabox hayo yamebaki kuwa yakifuga panya bila kutoa huduma iliyolengwa. Naamini wahusika walioanzisha huduma hii kwa lengo zuri ambalo lilikuwa ni kuhamasisha jamii itumie kinga ya kondomu katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi, magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.
Huduma hii ilikuwa ni bora katika kuisaidia jamii hasa wale watu wanaoogopa kwenda katika maduka kununua kondomu, Hivyo tunawaomba wahusika waweze kuendeleza huduma ili kuhamasisha jamii matumizi ya kondomu ili kupunguza maambukizi mapya yanayoongezeka siku hadi siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments: