Mshiriki wa Big Brother Africa 2012 kutokea Nigeria mwanadada Goldie Harvey amefariki dunia hivi punde. 

Taarifa ambazo tumezipata toka vyombo mbali mbali vya habari vya nchini Nigeria na hata kwenye kurasa yake katika mtandao wa jamii Facebook na Twitter zinasema kuwa Goldie alifariki muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo alikuwa anakwenda kwenye tuzo za Grammy.

Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia kurasa zake za twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria, hali yake ya afya ilibadilika ghafla ikabidi apelekwe hospitali ambako hakuchukua muda mrefu akafariki dunia.

 Taarifa nyingine zilizopatikana zinasema kuwa Msanii wa Kenya CMB Prezzo alikuwa ametua nchini Nigeria ili kwenda kusherekea shikukuu ya wapendanao.

Kajunason Blog inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na Msanii Prezzo ambaye alikuwa ni nchumba wake Godie.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: