Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti katika bustani ya Jumba la Rideau Hall jijini Ottawa katika siku ya pili ya ziara yake rasmi nchini Canada huku akishuhudiwa na Gavana Jenerali wa nchi hiyo Mhe David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi Octoba 4, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Otttawa Alhamisi Octoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimama wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi Octoba 4, 2012. Mbele yake ni baadhi ya veterani wa kijeshi waliohudhuria hafla hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi hayo wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya sanduku la Zanzibar (Zanzibar chest) Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, Alhamisi Oktoba 4, 2012
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: