Mgeni rasmi,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernald Membe akizindua albamu mpya wa Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kongo,(wa tatu kulia),Solomoni Mukubwa iitwayo KWA UTUKUFU WA MUNGU, na Kushoto ni Mkurugenzi wa Msama Promotions,Bw.Alex Msama,ambapo katika uzinduzi huo Waziri Membe na wajumbe wake wamechangia kiasi cha Shilingi Milioni 25,ambapo kiasi cha milioni 50 zilihitajika kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernald Membe akizindua albamu hiyo iliyojulikana kwa jina la KWA UTUKUFU WA MUNGU ya Solomoni Mukubwa,kushoto ni Mkurugenzi wa Msama promotions,Alex Msama,Solomoni Mukubwa pamoja na John Melele wakishuhudia tukio hilo adhimu jioni ya leo.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akiongozwa na Mkurugenzi wa Msama Promotion kuelekea jukwaani kwa ajili ya kuzindua albam ya Solomon Mukubwa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe wa pili kutoka kulia akiongozana na Alex Msama Mwandaaji wa Tamasha la Pasaka, kutoka ushoto ni Richard Kasesela Mwenyekiti wa kamati ya ushauri Madini na Askofu Gamanywa.


Rebbeca Malope akiwa na mwanamuziki mwenzake wa nyimbo za injili,Rose Muhando wakiwa wamezungukwa na washabiki wao wakiimba kwa pamoja jioni ya leo ndani ya tamasha la pasaka,uwanja wa Taifa,jijini Dar.
Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebbeca Malope akitumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la pasaka,ndani ya Uwanja wa Taifa,ambapo maelfu ya watu wamejitokeza kusherekea tamasha hilo lililofana kwa kiasi kikubwa.
 Rebbeca Malope akitumbuiza.
 Rebbeca Malope akiendelea kutumbuiza huku uwanja ukilipukwa kwa mayowe.

Rebbeca Malope akijiandaa kwenye kutumbuiza ndani ya tamasha la pasaka jioni ya leo.
 Rebbeca Malope akijiandaa kukwaa jukwaani.
 teknolojia nayo inachukua mkondo wake kwenye matukio.
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Zambia,Joshua Sekeleti akitumbuiza jukwaani jioni ya leo.
Mwimbaji nyota wa nyimbo za injili hapa nchini Rose Muhando akiwa na skwadi lake akitumbuiza jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la pasaka,ndani ya uwanja wa Taifa,jijini dar.

Mwanamuziki Solomon Mukubwa akiimba jukwaani kabla ya kuzindua albamu yake iitwayo KWA UTUKUFU WA MUNGU,ambayo imezinduliwa na mgeni rasmi wa tamasha la Pasaka,Waziri wa  Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernald Membe.
Anastazia Mukabwa akiwa na baadhi ya waimbaji wake wakifurahia wakati Solomoni Mukubwa alipokuwa akitumbuiza.
 Watu waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la pasaka jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Umati wa watu ndani ya uwanja wa Taifa kusherehekea tamasha pasaka.



Kikundi cha Glorious kikitumbuiza jukwaani.
Wimbo wa kiatu kivue ikiimbwa na wanamuziki Anastazia Mukabwa sambamba na Rose Muhando huku uwanja mzima ukilipukwa na mayowe.
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akizungumza na Wanahabari ndani ya Uwanja wa Taifa jioni ya leo kabla ya tamasha la Pasaka kuanza,Tamasha la pasaka limeandaliwa na kampuni ya Msama Promotions Ltd

Waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya wakittumbuiza jukwaani.
Waimbaji wa nyimbo za Injili wakiwasili ndani ya uwanja wa Taifa jioni hii,kutumbuiza tamasha la pasaka 2012,kulia ni Christina Shusho,Upendo Kilahilo pamoja na Upendo Nkone wakiwa na watoto wao. 
Mwanamuziki nyota wa muziki wa nyimbo za injili kutoka nchini Afrika Kusini,kati pichani akiwasili ndani ya uwanja wa Taifa,tayari kutumbuiza tamasha la pasaka jioni ya leo.
Malkia wa nyimbo za injili Rose Muhando akiwasabahi washabiki na wapenzi wa muziki wa kiroho alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa Taifa,kutumbuiza tamasha la pasaka.
Mwimbaji nyota wa muziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini DRC-Congo Solomoni Mukubwa akiwasili  kwenye uwanja wa Taifa jioni hii,huku akiwasalimia wapenzi na washabiki wa muziki wa injili hapa nchini waliofika kwenye tamasha la Pasaka.
 Sehemu ya wakazi kutoka sehemu mbalimbali wakiendelea kumiminika  kwenye uwanja wa Taifa kusherehekea tamasha la pasaka linaloendelea hivi sasa.
Wakifuatilia kwa makini yanayoendelea hivi sasa hapa Uwanjani,ambapo katika tamasha hilo mgeni rasmi ni Waziri wa mambo ya Nje Mh Bernad Membe.

 Maandalizi yakiendelea sehemu ya mafundi mitambo.
Sehemu ya jukwaa ambako wasanii wataonesha umahiri wao wa kuimba na kucheza huku wakimsifu Mungu.
 Baadhi ya kundi lwa wiambaji wakiwasili uwanjani hapa tayari kwa kutumbuiza ndani ya tamasha la pasaka.
Patanogaje uwanja wa Taifa ile live live le. 

Picha zote: Michuzijr Blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: