Wengine walipanda juu ya nguzo
 ilikuwa ni patashika nguo kuchanika

 Kila mmoja alibuni njia zake za kunasa tukio bila kupitwa

 Ama kweli Mungu ni mwema 
 Umati wa watu wakiwa wamejipanga Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kusubiri kupokea mwili wa marehemu Steven Kanumba. Ambapo watu wapatao 45,000 walijitokeza kumzika mpendwa wao.
 Kila mmoja alikuwa na majonzi.
 Simanzi zilitanda makabuni ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Umati wa watu ukiwa umehamaki
 Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu alikuwa ni gumzo msibani kule baada ya kuzingwa na watu.
 watu wakiwa wamemzingira
 ...watu walikimzingira Wema Sepetu
 Watu wakiwa wametanda makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 ...wakihangaika kutafuta lilipo kaburi 
 Mama yake Marehemu Steven Kanumba akiwa ameshikiliwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Wakizika..
 Marehemu Steven Kanumba.
 Mama yake Marehemu Steven Kanumba amuaga mwanae.
 ...Nenda kwa amani mwanangu
 Watu wakiwa na simanzi

Marehemu Steven Kanumba alizaliwa tarehe 8, January 1984, Kambarage Shinyanga akiwa mtoto wa tatu kutoka katika familia ya watoto watatu ya Charles Kanumba na mama Florence Angelo Mtegoa.

Marehemu Steven Charles Kanumba alikuwa muigizaji maarufu/nguli wa filamu wa Tanzania aliyeitangaza na kuipeperusha bendera ya nchi yetu Tanzania Kitaifa na Kimataifa kupitia maigizo.

Marehemu Steven Kanumba alijiunga na elimu ya msingi shule ya Kaboya, mkoani Kagera mwaka 1992 na baada ya hapo elimu  sekondari katika shule ya Mwadui, mkoani Shinyanga 1999-2000 aliposoma kabla ya kuhamia shule ya seminary Vosa mkoani Shinyanga mwaka 2001. Baada ya hapo alijiunga na elimu ya sekondari ya juu (A'level) mwaka 2003-2004 katika shule ya Jitegemee mkoani Dar es Salaam.

Marehemu Steven Kanumba alikuwa muumini mzuri wa dhehebu ka AIC anbapo alitumikia kanisa katika shughuli mbali mbali haswa za uimbaji wa kwaya katika kijiji chake cha Kambarage mkoani Shinyanga na baadae kujiunga na kwaya ya AIC Chang'ombe jijini Dar es Salaam ambapo umauti ulipomkuta. 

Marehemu Steven Kanumba alijiunga namaigizo mwaka 2002 kupitia kundi la sanaa la Kaole Sanaa Group, mwaka 2004 Marehemu Kanumba alihamia katika tasnia ya filamu kupitia kampuni ya Game First Quality hapo ukiwa mwanzo wa kuonja mafanikio. Mwaka 2009 Kanumba alifanikiwa kuanzisha kampuni yake ya KANUMBA THE GREAT FILM mpaka mauti yalipomkuta alisaidia kukuza vipaji na kuwezesha kupata ajira kwa vijana wengi waliopenda kujiendeleza kwenye fani hii.

Marehemu Kanumba alikuwa mshiriki mzuri wa shughuli za kijamii ambapo alitoa mchango wake sehemu mbali mbali kwa wahitaji na pia alifikia hatua ya mchango wake kuonekana katika makampuni ya kitaifa na kuchaguliwa kama mabalozi wa kuziwakilisha makampuni hizo zikiwemo Oxfam, kampuni ya Simu ya Zantel, Startimes n.k.

Marehemu Kanumba enzi za uhai wake alicheza filamu zipatazo 40 zikiwemo, Devil's Kingdom, Mosses, Uncle JJ, Red Valentine, Hero of the church, Big Daddy, Dar to Lagos, She's my sister, Cros my sin, This is it, Young Billionaire, Tambua Haki, Deception, Morning Alarm, JOhari, Sikitiko Langu, Unfortunate Love, Shauku, Crazy Love, A point of no return, Saturday Morning na nyinginezo nyingi.

Marehemu atakumbukwa kwa mengi sana, katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje nchi  na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchini mbali mbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa wa Kinajeria hapa nchini akiwemo Femi Ogdebede. Vile vile marehemu Kanumba alitunukiwa tuzo ya muigizaji bora wa Mwaka 2011/2012 ya ZIFF (Zanzibar Internatinal Film Festival). Kanumba alipata mwaliko kushiriki katika uzinduzi wa shindano la Big Brother Africa linalofanyika kila mwaka nchini Afrika Kusini mwaka 2010 ambalo Tamasha hilo lilihudhuriwa na watu maarufu barani Afrika, pia tamasha kubwa la Filamu la nchini Ghana ambalo linajulikana kama Festival of Film in Africa (FOFA 2012) lililofanyika katika mji wa Accra Ghana.

Marehemu Kanumba alipatwa na umauti usiku wa kuamkia tarehe 7 mwaka 2012 nyumbani kwake Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam. 

Marehemu hakuwahi kuoa wala kuwa na mtoto.
Movie ambazo hazojatoka ni "Ndoa Yangu ishaanza promo, The Price ambayo imeshabadilishwa jina.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: