Meneja Masoko wa TWENDE,Hamis Omary,akitoa maelezo kuhusiana na TWENDE,kulia Naomi Maro, mmoja wa wajasiriamali,katika mkutano na waandishi wa Habari,Hadees Dar-es- salaam.
 Meneja Mradi, Gloria Mongela, akitoa maelezo kuhusiana na TWENDE, kulia Naomi Maro, Mmoja wa wajasiriamali, katika mkutano na waandishi wa Habari, Hadees Dar-es- salaam.
 Naomi Maro,mmoja kati ya wajasiriamali, kulia, akiwa na Meneja Mradi na Meneja Masoko wa TWENDE wakijadiliana kuhusu TWENDE katika mkutano wa waandishi na habari, uliofanyika Hadees. 
Naomi Maro,mmoja kati ya wajasiriamali, kushoto ni meneja akitoa hoja kuhusu TWENDE,kushoto akiwa na Meneja Masoko wa TWENDE, katika mkutano wa waandishi wa habari, uliofanyika Hadees.
---
Huu ni mwaka wa pili wa TWENDE ambao utafanyika tarehe 15, 16 na 17 Septemba mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar-es-salaam

Tunategemea mahudhurio zaidi mwaka huu,katika hafla ya TWENDE kama njia ya mawasiliano, kuendeleza na kuwahamasisha wanawake katika biashara zao kitaifa na kimataifa alisema Gloria Mongela meneja mradi wa TWENDE.

TWENDE imedhamiria kuchangia kutangaza malengo ya milenia ya 1,3,5 na 8, ambayo ni kuondoa umasikini na njaa, kutangaza haki na fursa sawa kwa wote, na kuwahamasisha wanawake kwenye afya zao na kuwaendeleza uhusianao wa kudumu kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

”Ningependa kusisitiza Uma kuhudhuria kwa kiasi kikubwa na kutumia fursa hii ya TWENDE kuuendeleza ujuzi wakijisaliamali kwa kuuonyesha bidhaa na huduma zao na pia kuhudhuria kwenye semina.Tunategemea ushirikiano mkubwa sio tu kwa marafiki na familia bali kwa wanawake wote wajasiliamali na jamii ya watanzania kwa ujumla”. Alisema Meneja Masoko wa TWENDE, Hamis Omary

Malengo ya TWENDE ni kuwakuza kibiashara wajasiriamali wanawake nchini hii itasaidia muongezeko wa wanawake wuzalishaji na uwiano sawa kibiashara na kimasoko katika jamii iliyotawaliwa na Wanaume.

“Tunaomba taasis za fedha ,maendeleo ya wanawake na watoo, na mashirika yaliobobea katika maswala ya jinsia kushirikiana na TWENDE ili kuweza kutimiza malengo ya Melenia namba 1,3,5 na 8, kwa kuwahamasisha wanawake wajasililiamari, kuhudhuria maonesho na pia kusambaza taarifa kwa uma kiujumla”, aliongeza Mr.Omary.

Maonyesho ya TWENDE, ni bure kwa watu wote ,ambapo yatafunguliwa saa 4:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni, kuanzia tarehe 15-17 Septemba 2011.

“Ninafurahia TWENDE,kwasababu inatoa nafasi ya wajasiliamali kukutana na kuwasiliana,na pia kupewa muunguzo mzuri katika biashara. Alsema Naomi Maro,Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali,walioudhulia,mkutano wa Twende na waandishi wa habari.

Maonyesho hayo ya siku tatu yataambatana na semina ili kuweza kuwapa wajasiriamali wanawake mbinu za kuzishinda changamoto na kujiendeleza kibiashara.

TWENDE, imedhaminiwa na Daily News, Habari Leo, Perfect Machinery, Ultimate Security, Global outdoor systems and 361 Degrees. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: