CHAMA cha Waalimu Tanzania(CWT) kimesema kuwa kusudio la kutangaza mgogoro na serikali liko pale pale kama ilivyopitishwa na Baraza la Taifa la Chama kwa sababu hakuna hatua za makusudi zilizochukuliwa na serikali kukabilia na matatizo ya waalimu hasa wanaoidai.

Pia chama hicho kimetoa wito kwa watendaji wake kuwasilisha majina ya waalimu wanaodai kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa kwao.

Hata hivyo alisema kuwa wanachama wanaobwa kushirikiano na viongozi wao japo kuwa inaonekana kuwa ni usumbufu kwa kuwasilisha nyaraka mara nyingi bila ya kuyapatiwa ufumbuzi.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es salaam jana na Rais wa Chama hicho Bw. Gratian Mukoba (kushoto) alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusina na maazimio waliofikia walipokaa na serikali kujadili madai yao.

Alisema kuwa walimu wanatakiwa kuendelea kuwa na subira wakati majadiliana yakiendelea na serikali ili kujua hatma ya madeni yao baada ya kikao kilichopangwa kufanyika kabla ya mwezi huu kukamilika.

Alisema kuwa maazimio yaliyofikiwa na kikao hicho ni chama kiwasilishe majina ya waalimu wanaodai kwa kuzingatia format iliyokubalika ili kiweze kudhibitisha madai yaliyowasilishwa ya zaidi ya sh bilioni 29.2.

Alisema kuwa majina hayo yanatakiwa kuwasilishwa kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma kabla ya Agosti 15 mwaka huu nyaraka zenye majina ya walimu hao.

"Serikali ilikuwa na wasiwasi kuwa huenda wanaodai ni wale waliokwishalipwa au waliowasilishwa nyaraka zao na mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za serikali alikataa madai yao na aidha walikata rufaa wakakataliwa au hawakukata rufaa,"alisema Bw. Mukoba.

Pia alisema kuwa majina ya walimu waliokuwa wanastahili kupandishwa madaraja kwa miaka ya nyuma lakini hawakupandishwa mwaka jana wa fedha kwa madai kuwa mwajiri hakuwa na fedha, hawa ni walioanza kazi mwaka 2007, waliopandishwa madaraja kwa mwaka jana wa fedha.

Hata hivyo alisema kuwa serikali inatakiwa kuangali upya waraka wa utumishi wa Kumb. Na.C/CA.44/45/01/84wa Desemba 1 mwaka 2009 ambao umelalamikiwa sana na waalimu wanaojiendeleza.

Bw. Mukoba alisema kuwa ushauri uliotolewa kwa siku zijazo viongozi wa CWTngazi za Wilaya washirikiene na wakurugenzi kuhakiki madeni ya waalimu kila baada ya miezi mitatu ili kwa pamoja wabaini madeni mapema na taarifa iwe moja kuepuka uisumbufu unaojitokeza kwa sasa.

"Walimu wakumbuke kuwa kuwasilisha madai huku akijua kuwa si madai halali ni kosa la jinai na atakayebainika mwajhiri wake atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani,"alisema Mukoba

Alisema kuwa Pande zote mbili kwenye kikao hicho kilikubalina kuwa serikali itaitisha kikao kingine kabla ya Agosti 30 mwaka huu baada ya CWT kuwasilisha majina Agosti 15 ili kwa pamoja pande zote zipitie na kuona ukubwa wa tatizo la madai ya waalimu kama yalivyowasilishwa, baada ya kukusanya madeni kutoka mikoani na kikao hicho ndicho kitatoa hatma ya utekelezaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: