Nchi ya Uchina imesema itaunga mkono uanachama wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa.
Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uchina Bwana Yang Jiechi wakati wa mkutano uliofanyika huko Beijing na ujumbe wa Palestinian ukiongozwa na  Bwana Azzam al-Ahmed, mjumbe wa Kamati ya utendaji ya Chama cha Fatah na Bwana Bassam al-Salhi, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi wa Palestina (PPP).
Waziri huyo alisisitiza msimamo wa nchi yake kuona kwamba Wapalestina wanapewa haki yao ya msingi ya kuwa wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Alisema Uchina ni miongoni mwa nchi za mwanzoni kabisa kukitambua Chama cha Kupigania Uhuru wa Palestina (PLO) na kwamba upo uhusiano wa kweli baina yake na chama hicho.
Jiechi aliongeza kusema kuwa Uchina itaendelea kushirikiana na Palestina katika majukwaa yote ya kimataifa ili hatimaye nchi hiyo ipate uhuru wake kamili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: