Waziri wa mambo ya kigeni wa Norway Bwana Jonas Gahr Stoere na mwenyekiti wa Mamlaka ya Palestina Bwana Mahmoud Abbas jana walitiliana saini makubaliano ya kuufanya ubalozi uliopo Oslo kuwa ofisi kamili ya kibalozi.

Bw. Stoere na Bw. Abbas walisaini hati za makubaliano hayo huko Oslo baada ya kumaliza kikao chao kuhusu hali ya mgogoro wa Mashariki ya Kati  na suala la Palestina kutaka kuungwa mkono kwenye Umioja wa Mataifa baadaye Septemba mwaka huu.

Stoere, ndiye alitangaza uamuzi huo wan chi yake alisema: “Uamuzi wa kuupandisha hadhi ubalozi wa Palestina katika nchi yake ni jambo la kufurahisha sana.”

Ofisi hiyo ya PLO mjini Oslo ilianzishwa mwaka 1994 kuwawakilisha Wapalestina katika nchi hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: