Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kilombero limemsimamisha kazi Mhandisi wa Wilaya hiyo Eng. Augustino Kiyaka kwa kushindwa kusimamia miradi mbalimbali ya ujenzi ya Halmashauri hiyo ambayo imegharimu mamilioni ya fedha.
Akitangazwa kusimamishwa kwa Mhandisi huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Ramadhani Kiombile alisema uamuzi huo umetokana na kamati ya nidhamu kuamua kumvua ukuu wa idara na kumsimamisha kazi kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ukuu wa idara na mshauri mkuu wa uhandisi katika Wilaya hiyo.
Kiombile alisema kutokana na hali Kamati ya nidhamu imempendekeza Eng. Godfrey Mbena ambaye ni Mhandisi wa idara ya ujenzi kukaimu nafasi hiyo wakati halmashauri ikisubiri maamuzi kutoka tamisemi ambao ndio mwajiri wake.
Baadhi ya miradi iliyolalamikiwa na wananchi kujengwa chini ya kiwango ni miradi ya madaraja matatu yaliyopo kijiji cha Miembeni, nyumba ya mganga kiongozi katika kijiji cha Taweta, mradi wa soko uliopo kijiji cha Chita na Banio katika kijiji cha Zinginali.

Toa Maoni Yako:
0 comments: