Watu tisa kati ya kumi na mmoja waliofariki na kujeruhiwa baada ya gari aina ya coaster kugongana uso kwa uso na Fuso katika eneo la daraja la barabara ya KIBOSHO wilayani MOSHI mkoani Kilimanjaro imetambuliwa.

Mkurugenzi wa huduma za wauguzi katika hospitali ya KCMC REDEMTA MAMSERI amesema  kati ya watu waliofariki wanaume ni tisa na wanawake ni wawili na kueleza kuwa majeruhi saba kati ya ishirini na nne waliolazwa katika hospitali hiyo hali zao ni mbaya na wamelazwa katika chumba maalum cha uangalizi.

Maiti waliotambuliwa katika ajali hiyo wamo pia madereva wa magari yaliyopata ajali hiyo JUDICA NDEONANSIA ambaye ni deva wa LIM SAFARI na Sifael Ndewario Kaaya Mkazi wa MERU ambaye ni dereva wa Fuso.

Wengine ni SIFAEL ROGATH, JOEL JOSEPH, DANIEL MACHA, AMIDO DAUD, WILFERD DAUD, MARIAM BAMIDI wote wakazi wa Machame Nshara na Halifa Mohamed mkazi wa Sadala.

Kwa upande wake Afisa upelelezi mkoa wa Kilimanjaro OBADIA NSELU amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa costa ambaye aliyapita magari mawili katika eneo hilo lenye daraja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: