Ni safari ndefu sana hadi kufikia sehemu ambayo wengi wanaiona kuwa ni mafanikio Kuna vikwazo, milima na mabonde lakini naamini njia ilionyooka haifunzi mengi Njia yenye drama, vilio na vicheko baadae ina hata hadithi ya kusimulia.

Kuna tulioanza nao lakini wakaishia njiani hawapo tena Kuna walioondelea mpaka leo wapo. Kuna waliotukutia njiani pia safari hawakuiweza Na kuna wapya ambao bado tunao mpaka sasa
Kuna waliopata nafasi nzuri zaidi sehemu nyingine na wakaondoka kwa amani pia tuliwatakia kila kheri
Yote hii ni safari tu

Hadithi hii tutaisimulia rasmi ndani ya Nyumba ambayo ilikuwa ni ndoto iliogeuka kuwa kweli Nyumbani Lounge, Ijumaa tar 22 July 2011 Uongozi wa Machozi Band utatoa tuzo kwa wanamuziki na wafanyakazi wa Band yake
Kwa:
Muimbaji Bora
Mfanyakazi Bora
Mwanamuziki mwenye nidhamu
Mwanamuziki aliedumu kwa muda mrefu na Band
Mwanamuziki mwenye Talent zaidi
na nyinginezo

Trophy na fedha taslimu zitakabidhiwa kwa wahusika baada ya hapo kila Ijumaa na Jumapili MACHOZI BAND itakuwa inapiga Nyumbani Lounge Tumehama Mzalendo.

Kutoka kwa;
Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: