Mwanamuziki Ludacris akizungumza jioni hii ndani ya hoteli ya Kilimanjaro-Kempinsk mara tu alipowasili jiji Dar..Ludacris ameahidi kukamua vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.

Operation Manager wa kampuni ya Prime Time Promotions/Clouds Media Group, Balozi Kidamba akiongozana na mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli ya Kilimanjaro -Kempinsk jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onesho lake moja ndani ya viwanja vya Lidaz Club jijini Dar.

 
 Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya Hip Hop, ambaye pia ni muigizaji wa Filamu ajulikanae kwa jina la Christopher Bryian Bridges a.k.a Ludacris akiwasili leo jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kupokelewa na Wenyeji wake. Mwanamuziki huyo ambaye ameletwa nchini na Kampuni Bingwa ya Burudani hapa nchini Prime Time Promotions Ltd/Clouds Media Group na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake maalum cha Serengeti kwa ajili ya tamasha la Serengeti Fiesta 2011 linalotakiwa kufanyika Jumamosi July 30, 2011 katika viwanja vya Lidaz Club jijini Dar es Salaam. 
Picha kwa hisani ya Michuzijr Blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: