Ni safari ya mwisho ya mazishi ya Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd Marehemu Danny Mwakiteleko Danny Mwakiteleko katika kijiji cha Ndala Mwakaleli wilayani Rungwe.

Ambapo misa ya mazishi ya Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd Marehemu Danny Mwakiteleko iliyofanyika katika kanisa la Kilutheri la Usharika wa Ndala Mwakaleli Dayosisi ya Konde, Marehemu Danny Mwakiteleko amezikwa leo kijijini kwao Ndala Rungwe Mkoani Mbeya na kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, waandishi, wahariri wa vyombo vya habari habari na watu mbali mbali.

Mke wa Marehemu Danny Mwakiteleko akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu mume wake.

Marehemu Danny Mwakiteleko alifariki kwa ajali ya gari wiki iliyopita ameacha Mjane na watoto wawili Caroline (14) na Vanesa (11) Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jackson Msome akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Danny Mwakiteleko mara baada ya mazishi.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: