Bunge la Ubeligiji, jana lilitoa wito wa kulitambua taifa la Palestina baada ya kikundi cha kijammi kuwasilisha muswada ambao unaitaka serikali ya nchi hiyo na zingine za Jumuia ya Ulaya kuitambua Palestina kama taifa kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967.

Leila Chahid, kiongozi wa kikundi hicho kwenye jumuia ya Ulaya, ameusifu msimamo huo wa Ubelgiji na Luxembourg, kwa kupitisha azimio hilo la kuitambua Palestina.

“Ni matarajio yetu kuwa serikali za nchi hizo zitazingatia matakwa ya watu wao ambao wanaunga mkono uhuru wa taifa la Palestina kwa misingi ya haki, usawa na uhuru kamili ili kuwe na utulivu katika ukanda mzima,” alisema.

Muswada huo ulipitishwa na wajumbe 43, 11 hawakushiriki kupiga kura; hakuna hata mmoja aliyepinga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: