Muonekano wa barabara ambayo ni vumbi tupu.Hapa ilibidi nipate picha ya ukumbusho tu.'Sijui tunafanyaje sasa'Muonekano wa basi mzuri ila ingia ndani ujionee mwenyewe...abiria wamebeba mpaka kuku.Duh! itakuwaje leo hapa porini, abiria wakiongea.Aha! Ama kweli tembea uone...Hapa abiria wakijadiliana cha kufanya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuharibika porini.
Kweli ule usemi waliousema wahenga kuwa msafiri kafiri, uliweza kutukuta jana jioni wakati tukiotokea Dar es Salaam kwenda mjini Tabora. Ama kweli wenzetu wanaonekana matatizo haya ya barabara na ubovu wa magari wamezoea kwa vile pindi gari linapoharibika wao huwa wanaonekana kuwa na moyo wa subira tofauti na wageni wengine ambao husafiri kwa mara ya kwanza na magari hayo.
Nilisikia kauli moja ambayo aliitoa mzee mmoja ambaye alionekana ni mgeni na mazingira ambayo gari tulililokuwa tuisafiria liliharibika, "Hivi kweli mwenyezi Mungu amekukosea nini mpaka kuja kukukabisha huku ambapo hakuna huduma za jamii, kwanza barabara zenyewe ovyo", hayo ni maneno yake huyo mzee. Kifupi barabara ya kutoka Nzega kwenda Tabora mjini ni takribani kilometa 117 ila magari yanasafiri kwa masaa yapatayo 4 mpaka 6 hali ambayo kwakweli si haki.
Hizo picha zinaonyesha jinsi abiri wanavyohangaika na kuwaza cha kufanya wakati gari tulilokuwa tukisafiria kuharibika njiani tena porini.
Hizo picha zinaonyesha jinsi abiri wanavyohangaika na kuwaza cha kufanya wakati gari tulilokuwa tukisafiria kuharibika njiani tena porini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: