Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel ikisaidiwa na klabu ya Manchester United ya England leo imezindua mpango maalum wa soka wenye lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.

Mpango huo unajulikana kama Airtel Rising Stars uzinduzi wake uliofanyika katika shule ya sekondari Makongo umehudhuriwa na mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Manchester United pamoja na timu ya taifa ya England Andy Cole.

Mradi huo wa kuibua vipaji unahusisha bara zima la Afrika kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wanasoka chipukizi chini ya umri wa miaka 17 kuonyesha uwezo wao mbele ya mawakala wa soka, makocha na kupata fursa ya kujiendeleza zaidi ambao unawalenga wavulana na wasichana kwa nchi nzima.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Andy Cole amesema ni furaha kwake kuwepo hapa nchini ambapo lengo kubwa ni kuja kuzindua mpango wa kuibua vipaji ya Airtel Rising Star na anaamini anaweza kuleta kitu kitakacholeta mabadiliko kwa wachezaji.Cole aliendelea kwa kusema nje ya kuja kama mchezaji wa zamani wa Manchester United lakini binafsi amefuraia kuja kwenye ardhi ya Tanzania.

Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Fenella Mukangara amesema kwamba mpango huo utaongeza msukumo katika mkakati wa maendeleo ya michezo nchini ambapo wao kama Serikali inapongeza mpango huo.

Zoezi hilo litahitimishwa kwa kliniki ya soka ya aina yake itakayofanyika nchini Gabon na Tanzania chini ya usimamizi wa jopo la makocha kutoka katika klabu ya Manchester United ya nchini England.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: