Baraza la usalama la Israel siku ya Jumatatu liliidhinisha mpango wa jeshi la wanamaji kuzuia msafara wa meli zinazopeleka misaada huko Gaza kwa kisingizio kuwa zinahalifu amri ya kutoingia Gaza.
“Baraza hilo la mawaziri limepitisha mpango huo kuzuia misaada hiyo kuingia Gaza bila ya idhini,” ilisema taarifa ya habari.
Habari hiyo ya redio iliongeza kuwa mawaziri walibadilisha msimamo wao wa kuwaadhibu waandishi wa kigeni wanaoambatana na msafara huo kupigwa marufuku kuingia Israel kwa miaka 10.
Takriban wanaharakati 350 kutoka nchi 22 wanatarajia kujiunga na msafara huo wenye meli kumi unaoitwa “Msafara wa Uhusu” (Freedom Flotilla II).
Miongoni mwao ni mwandishi maarufu wa riwaya kutoka Sweden Bw Henning Mankell, pamoja na waandishi. Wote hao wataelekea Gaza licha ya amri ya miaka mitano sasa iliyowekwa na Israel ya kutoingia Gaza ambako wanaishi Wapalestina milioni 1.5.
Toa Maoni Yako:
0 comments: