Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Rafael Ndunguru akihojiwa.Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando (kushoto) akifafanua juu ya zoezi hilo ambalo alisema litakuwa linafanyika kila jumamosi ya kwanza ya mwezi lengo lake kuu ni kuweka jiji safi.Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa katika zoezi la kufanya usafi kuhakikisha jiji linakuwa safi lililofanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.Wafanyakazi wa tigo wakichukua vifaa tayari kufanya usafi.Usafi ukiendelea.Wanachi mbali mbali wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika usafi.Wanafunzi na watu mbali mbali walijotokeza.Askari wa JKT waliungana katika zoezi hilo la usafi.Askari wa JKT waliungana katika zoezi hilo la usafi.
Katika mkakati wa kuhakikisha mazingira ya jiji la Dar es Salaam yanakuwa katika hali ya usafi wakati wote, Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imetoa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dar es Salaam, vyenye dhamani ya shilingi milioni nne.
Vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa ni pamoja na mafyekeo, Reki, Koleo na mifuko ya kuzolea taka.
Katika makabidhiano hayo ambayo yaliendana na zoezi la kufanya usafi katika sehemu mbali mbali ya jiji la Dae es Salaam ambapo zoezi hilo lilifanywa na askari wa JKT, askari wa jiji la Dar es Salaam, wanafunzi wa shule za sekondari mbali mbali za Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Tigo.
Nae ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando alisema kuwa mbali na kuboresha huduma kwa wateja wake, kampuni hiyo inamambo mengi ya kuwafanyia watanzania.
Aliongeza kuwa Tigo Inayofuraa kuona watanzania wanaishi katika mazingira mazuri ili waweze kupata afya njema kwa ajili ya kuwajibika katika shughuli mbali mbali.
Safisha jiji programu ya endelevu ambayo ilitangazwa na ofisi ya makamu wa Rais kuwa kila jumamosi ya kwanza ya mwezi kuanzia saa 1.00 asubuhi mpaka saa 4.00 asubuhi ni siku ya kufanya usafi katika miji mbali mbali hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: