Mgeni rasmi, Makamu wa Rais akisoma hotuba fupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tuzo za kumsaka Mwanamichezo Bora 2011, ambazo zimedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa, akipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) kimempa mzee Mkapa tuzo hiyo maalum ya heshima, kutokana na mchango wake katika michezo hasa ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa, Mh Mkapa amesisitiza uwanja huo uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo, pichani kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda. Katika utoajiwa tuzo hizo mchezaji wa jumla ni Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa Netball katika timu ya JKT
Mbweni.Mwanamichezo bora wa jumla katika utoaji wa tuzo hizo Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa Netiboli katika timu ya JKT Mbweni, akipokea tuzo yake kutoka kwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Mh. Dk. Mohamed Gharib Bilal, mara baada ya kutangazwa rasmi na kujinyakulia gari aina ya Toyota GX 100, iliyotolewa na Chama cha waandishi wa habari za michezo *TASWA) na wadhamini wa tuzo hizo Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), kushoto ni waziri wa Habari, Vjiana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi. Picha zaidi na MICHUZI JR.
Home
Unlabelled
MWANAMICHEZO MWANAIDI HASSAN AIBUKA KINARA TUZO ZA TASWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments: