Mnara wa Azimio la Arusha ambao umebeba picha zote za chini.
Kilimo cha mkono.
Kilimo cha jembe la ng'ombe.
Ushirikiano katika kujenga na kuonyesha usawa kati ya mwanamke na mwanaume.
Kilimo cha matrekta.
Picha ya juu ni mnara wa Azimio la Arusha ambao ndiyo unaitambulisha jiji la Arusha. Itambulike kuwa Azimio la Arusha lilikuwa na lengo la Ujamaa na Kujitegemea kama unavyoona hizo picha ambazo zimo pembeni kwa mnara huo.

Mnara huo wa Azimio la Arusha ulikuwa na madhumuni ya kuwafanya watambue kuwa:

(a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
(b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;
(c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya
kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya
Mikoa hadi Serikali Kuu;
(d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo
yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na
wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;
(e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii
hifadhi ya maisha yake na ya mali yake aliyonayo kwa
mujibu wa Sheria;
(f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki
kutokana na kazi yake
(g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili
wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana
kwa vizazi vyao;
(h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda
sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia
muhimu za kuukuza uchumi; na
(i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,
kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili
kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya
mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine
na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani
na siasa ya watu wote kuwa sawa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: