Mwimbaji aliyeimba wimbo wa kivue kiatu Anastazia Mukabwa kutoka nchini Kenya akishirikiana na Rose Muhando akikivua kiatu mbele ya mashabiki wake.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Muhando akikonga nyoyo za mashabiki wake katika uwanja wa CCM Kirumba jana.Mwimbaji wa muziki wa injili, Bonny Mwaitege akiimba katika tamasha la muziki wa injili lililofanyika jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kukamilisha ratiba ya matamasha hayo, ambayo yalianza jumapili iliyopita jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee, huku rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwa mgeni rasmi, yakifuatiwa na Dodoma katika uwanja wa Jamhuri siku ya jumatatu na kumalizika jana. Umati mkubwa ulifurika katika uwanja wa CCM Kirumba na ulikuwa ni wenye furaha kwa kupata burudani hiyo, kutoka kwa waimbaji wa muziki wa injili mbalimbali ambao ni wakubwa katika nchi za Afrika Mashariki, Bonny Mwaiteje ameimba nyimbo zake kadhaa kama vile Mama ni mama , Njoo Ufanyiwe maombi na nyingine.

Ukitaka kuangalia picha zaidi tembelea: FullShagwe Blog

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: