Wafanyabiashara ya mkaa wamenyooshewa kidole kutokana na mbinu mpya inayoinyima mapato halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Pwani kwa kupitia kwenye njia za panya wakiwatumia madereva wa pikipiki na baiskeli.

Akifunga kikao cha kupitisha bajeti ya wilaya hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Magahila pamoja na kuwapongeza watumishi wanaokaa kwenye vituo vya ukaguzi wa maliasili kwa udhibiti wao na akawataka madiwani wenzake kutoa ushirikiano katika kuhakikisha wahujumu hao wanakomeshwa.

Magahila ambaye pia ni diwani wa Kata ya Panzuo alisema wamejipanga kuongeza vyanzo vya mapato na kuvilinda vilivyopo ili mkakati wa kuipaisha wilaya kwenye medani ya maendeleo uzae matunda hali itakayofanikisha wananchi wauage umaskini.

Mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni katibu wa baraza alisema kipimo cha utendaji kazi wa watendaji kata na vijiji kinaendana katika kuwadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wasaliti hao wa maendeleo kwa kuwashirikisha Idara ya Maliasili na Jeshi la Polisi waliopo vituoni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: