Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi –Zanzibar
Mkazi mmoja wa MwananyamalaJijini Dar es Salaam, Bw. Abdallah Nassoro maarufu kama Mzee wa Shamba, amejikuta akijisalimisha, katika Kituo Kikuu cha Polisi Madema mjini Zanzibar ili kujinusuru na athali za utumiaji wa dawa la kulevya.
Bw. Abdallah ambaye ni mtumiaji mzoefu wa dawa za kulevya alipofika Polisi alisita kuingia ndani ya Kituo kwa kuhofia kutiwa nguvuni na Makachero wa Polisi ambapo alilazimika kusimama nje na kumuomba Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi SP Mkadam Khamis Mkadam, kutoka nje ili amsikilize shida yake.
Hata hivyo kutokana na busara za Mkuu huyo wa Polisi wa Wilaya (OCD), alikubali kutoka nje ya Ofiisi yake kwenda kumsikiliza mteja huyo nje ya ofiisi kama alivyoomba na ndipo mteja huyo alipotoboa siri kuwa madawa hayo yammfanya kumtelekeza mkewe na watoto wawili huku akingali anampenda.
Amesema amelazimika kupanda katika meli ya Aziza kwa kificho na kufika Zanzibar kuomba msaada wa kupatiwa tiba ya kuachana na dawa hizo ambazo amesema zimekuwa zikimletea maumivu makubwa mwilini na kumlazimisha kuiba chochote kitakachokuwa mbele yake hata kama ni mali yake ili akiuze aweze kununua dawa hizo.
Amesema ili kuhakikisha kuwa dawa za kulevya ni hatari, kwa upande wake aliyeanza kutumia tangu mwaka 1991 mbali ya kusababisha yeye kuachana na mkewe na kuwatelekeza watoto wake wawili, lakini pia amefarakana na kutengwa na ndugu, jamaa na marafiki zake.
“Kaka kama una motto ama ndugu yako, mwambie usithubutu sio kutumia lakini kuonja dawa za kulevya ni hatari kubwa na atakayeonja hataweza kuacha kwa urahisi kwa vile zitakulazimisha kuendelea kuzitumia na ukiacha utaumwa na tumbo, vichomi mwili mzima na kuharisha nap engine kupoteza maisha yako mapema”. Alisema huku akimtahadharisha Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Unguja.
Kwa upande wake Mkuu huyo wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Unguja SP Mkadam, alimpongeza Mzee wa Shamba kwa kujitoa kuachana na dawa hizo ingawa kwa sheria mpya ya Zanzibar ingemfanya apelekwe Mahakamani na kuhukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita jela.
Hata hivyo SP Mkadam alimwelekeza mtu huyo kwenda katika kitengo cha Polisi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kupata ushauri nasaha pamoja na maelekezo mengine kuhusiana na tatizo lake.

Toa Maoni Yako:
0 comments: