KUHUSU MATALUMA

Mataluma anajulikana kwa ngoma yake maarufu sana “Kariakoo”, Mataluma ni moja kati ya wasanii wengi ambao wapo ndani ya nyumba ya vipaji (T.H.T),mataluma anajulikana kwa anina ya ngoma zake ambazo zinachezeka sana na kupendwa kusikilizwa na watu wengi.

Mataluma alizaliwa Mkoani Dodoma na kuanza sanaa kama mchezaji pale T.H.T Mataluma alipenda kucheza lakini mwisho wake alijikuta akipenda vyote; yaani kucheza na kuimba pia.
Mataluma mwenye staili ya pekee
katika utunzi wa ngoma zake zinazochezeka na kugusa maisha ya watu ya kila siku na kuchanganya na midundo inayochezeka.

Kama hiyo haitoshi Mataluma anapenda muziki na kukaa kitaa, ndio maana mziki wake unagusa kitaa kwa njia mbali
mbali na ni ambaye ameleta tena aina ya muziki ambao ulikuwa unapotea.
Ngoma yake ya Kariakoo ni kuhusu eneo la Kariakoo ambapo ni maarufu kwa wizi mdogomdogo wa mifukoni, ambapo wengi wetu tumeathirika nao kwa upande mmoja au mwingine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Huu wimbo ni KIBOKO! Big up sana kwa kijana Mataaluma! Amenikosha sana!

    ReplyDelete