
Ndumbalo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za shirikisho la mpira wa miguu TFF zilizoko Karume jijini Dar es salaam, na kuongeza kuwa benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na kocha wa timu hiyo Pelle Olsson limemkubali mchezaji Haruna Moshi na kuamua kumsajiri, hivyo amerudi nyumbani ili kutoa nafasi kwa timu hiyo ya Gefle FC kufanya mazungumzo na Simba timu ambayo Haruna Moshi amekuwa akiichezea.
Ameongeza kuwa hata hivyo kuna kila dalili kwamba mazungumzo kati ya Simba na Gefle FC yanaenda vizuri na kutakuwa na mafanikio katika mazungumzo hayo ili Haruna Moshi aweze kurejea nchini Sweden na kujiunga na timu hiyo ili kukamilisha taratibu zingine ikiwa ni pamoja na kusaini mkataba.
Haruna anatakiwa kuwa Sweden kabla ya januari 4 wakati msimu wa ligi ya nchi hiyo utakapokuwa unaanza.
Wakala huyo amesema kwa upande wa mchezaji Joseph Kaniki ambaye waliondoka na Haruna Moshi yeye pia amefanikiwa na kusaini mkataba wa miaka miwili hivyo kinachasubiriwa nia ITC yake ambayo inatakiwa kutumwa nchini Sweden na Shirikisha la Mpira wa Miguu nchini Rwandaambako Joseph Kaniki alikuwa akicheza mpira wa kulipwa
Toa Maoni Yako:
0 comments: