Mlima Kilimanjaro, Fahari ya Tanzania.
Watanzania wamehamasishwa kujitokeza kupigia kura Mlima Kilimanjaro ili uweze kushinda katika maajabu saba mapya ya dunia yatakayofanyika tarehe 11 Novemba 2011 Lisbon Ureno.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dare es salaam Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Save Mt.Kilimanjaro Bw.Ernest Olotu amesema mlima Kilimanjaro ulipendekezwa kuingia kwenye mashindano ya maajabu saba mapya ya duniani. tarehe 7/7/2007.

Akielezea kuhusu mashindano hayo Bw. Olotu amesema shindano la Maajabu saba mapya ya duniani yalizinduliwa na shirika la New Open World Cooperation (NOWC) tarehe saba mwezi wa saba Lisbon Ureno ambapo kura zaidi ya milioni 100 zilipigwa kutafuta maajabu 28 mapya ya dunia.

Mwenyekiti huyo ameelezea kuwa vivutio 77 vilipendekezwa mwanzoni ambapo 28 vilipigiwa kura kuingia kwenye shindano hilo”,Afrika ikitoa nchi mbili Tanzania inayoshindanisha mlima Kilimanjaro pamoja na Afrika kusini inayoshindanisha Table Mountains.

Aidha Bw Olotu amesema Mlima Kilimanjaro una nafasi nzuri yakushinda kuingia katika maajabu hayo kama utapigiwa kura nyingi kutoka kwa watanzania.

“waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari mlioko hapa na wasiokuwepo hapa ni jukumu letu kuwahabarisha na kuwahamasisha Watanzania wote popote waliko bila kujali itikadi,dini ,rangi wala kabila kuonyesha uzalendo tushirikiane pamoja katika kupiga kura ili kuhakikisha Mlima Wetu unashinda”.alisema Bw.Olotu.

Amesema watu watakaotaka kupiga kura waingie kwenye tovuti ya http://www.smk.or.tz kupata maelezo ya kupiga kura au wanaweza kuingia moja kwa moja kwenye tovuti ya http://www.new7wonders.com

Sambamba na mtandao namba za simu zitakazotumika kupiga kura kimataifa kutokea nchini ni +2392201055,+18697605990,+16493398080 na +447589001290.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: