Articles by "SHERIA"
Showing posts with label SHERIA. Show all posts

Baadhi ya wananchi hawana elimu ya kutosha kuhusu demokrasia, demokrasia imeambatana na uhuru wa kujieleza, haki za msingi na mambo mengine! Demokrasia ni aina ya utawala ambapo madaraka yako mikononi mwa wananchi, ama moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi waliowachaguliwa.

Demokrasia na utu ni viini vya jamii yenye haki na maendeleo. Demokrasia inatoa mfumo wa utawala wa haki, huku utu ukilinda haki na heshima ya kila mtu.

Kumkashifu, kumtukana na kumvunjia heshima kiongozi au mtu yeyote, ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi nyingi duniani. Tanzania kanuni ya adhabu kifungu cha 89(1)(a)(b) kinasema, "Mtu yeyote ambae anatumia lugha chafu, ya matusi au ya usafihi kwa mtu mwingine yoyote kwa namna ambayo huenda ikaleta uvunjifu wa amani au anazozana au, kwa namna nyingine yoyote, ataleta fujo kwa namna ambayo huenda ikaleta uvunjifu wa amani, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miezi sita".

Tusichanganye hili Mf: Ukasimama ukaeleza umuhimu wa kutengeneza hospitali kabla ya barabara ni bora zaidi kuliko kumueleza kiongozi unanenepesha tumbo barabara hujengi. Utu wake, mambo yake binafsi yanahusiana nini!!

Demokrasia ni utu si lugha ya matusi, demokrasia ni kujali faragha za wengine, Demokrasia inategemea mazungumzo ya heshima, mawasiliano ya uwazi na haki ya kila mtu kushiriki bila kuhisi uonevu, chuki au vitisho. Vyombo vya kusimamia sheria huchukua hatua endapo mtu amedhalilishwa au kutukanwa, wananchi wanaaminishwa na baadhi ya watu kwamba huko ni kutokuwepo kwa demokrasia jambo ambalo si sahihi!!

Ukitoa lugha ya kashfa, matusi ukategemea utaachwa, huo ni uvunjifu wa sheria.

Na: Mwanasheria Ally Babu (LL. B, LL.M – International Criminal Justice) 0767126969