Na Oscar Assenga, Muheza.
BENKI ya NMB nchini imetoa imechangia vifaa vyenye thamani ya Milioni 60 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya elimu kwa shule tano za Msingi katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali
Msaada huo ulikabidhiwa kwa Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko na Afisa Mkuu wa Udhibiti wa Benki ya NMB Doreen Joseph katika Halfa iliyofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayanu humo katika wakati Juma la Elimu uliokwenda sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Mtoto wa leo Samia wa Kesho.
Alivitaja vifaa hivyo ambavyo benki hiyo imechangia kuwa ni Madawati 200 kwa shule ya Msingi Kwemkamba, Magusuru, Mdote, Ngomeni na Mwembeni ambapo kila shule itapata madawati 50 ,vifaa yengine ni vitanda 40 vya double deka na magodoro 80 kwa ajili ya shule ya Msingi Ngomeni.
Alisema pia wamekabidhi vitanda 32 na magodoro 64 kwa ajili ya msingi Masuguru ambayo vitakuwa chachu katika kuhakikisha wanatatua changamoto ambazo zilikuwepo awali katika shule hizo.
“Nikushukuru Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko pamoja na Serikali kwa kazi kubwa inayofanywa kuendelea kuleta maendeleo nchini na sisi Benki ya NMB tupo tayari kushirikiana na Serikali katika kuendeleza maendeleo”Alisema .
Aidha alisema kwamba utoaji wa vifaa hivyo ni sera ya Benki hiyo kuendelea kurudisha kwa jamii ambayo ni sehemu ya faida wanayoipata kama benki inatoka kwa wadau na jamii hivyo hiyo sehemu yao wanatakiwa kurudisha kwa jamii.
“Benki ya NMB inatambua juhudi za serikali katika kusimamia elimu kwa nguvu zote zilizowekwa ili kuboresha utoaji wa mijini na vijiji ikiwemo utoaji wa elimu bure tunaipongeza Serikali kwa hilo sisi kama wadau furaha yetu ni kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kuisaidia jamii yetu”Alisema
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko alisema kampeni hiyo ya Mtoto wa leo ni Samia wa kesho muhimu ambayo inaonyesha walivyoamua kuwekeza kwenye msingi wa muhimu wa watoto kujiamini na hatimaye kuweza kutimiza ndoto ya kuwa viongozi bora wa baadae.
Naibu Waziri Mkuu huyo aliwataka pia wazazi na walimu kushirikiana kuwaandaa wanafunzi wao kuwa viongozi na wazazi bora kwa siku zijazo huku akieleza kwamba Serikali imewekeza katika sekta ya elimu ili kupata matokeo na maendeleo yanayoendana na uwekezaji huo.
Naye kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Zainabu Katimba alisema Serikali imejipanga kuwaandaa viongozi bora wa kesho kwa kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu na miundombinu mbalimballi ikiwemo mazingira bora ya kujifunzia.
Toa Maoni Yako:
0 comments: