Waziri wa Michezo,Sanaa na Utamaduni Dkt Damas Ndumbaro kushoto akimkabidhi Kombe la Mashindano ya Odo Ummy Cup Nahodha wa timu ya Kiomoni FC mara baada ya kuibuka Mabingwa kwa kuifunga Nguvumali FC penati 3-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga juzi ambapo mshindi huyo alipatiwa pia kitita cha Sh Milioni 3,pikipiki ya magurudumu matatu,Ng’ombe,Jezi Seti pamoja na mpira kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya ambaye ndie muandaaji wa Mashindano hayo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman
Na Oscar Assenga, TANGA
TIMU ya Kiomoni FC wametawazwa kuwa Mabingwa wapya wa Michuano ya Kombe la Odo Ummy Cup baada ya kuibamiza timu ya Nguvumali FC penati 3-1 katika mchezo wa Fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga.
Kutokana na ushindi huo waliweza kujinyakulia kitita cha Sh.Milioni 3,Pikipiki yenye Magurudumu matatu,Ng’ombe,Jezi Seti pamoja na mipira huku Mshindi pili timu ya Nguvumali FC waliweza kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 2.5 na Mpira na Jezi Seti 1.
Michuano hiyo ya Odo Ummy Cup huchezwa kila mwaka kwa kushirikisha kata zote za Jimbo la Tanga yakiwa na lengo la kuibua vipaji na kukuza kiwango cha soka kwa vijana ambao kupitia mpira wanaweza kujikwamua kiuchumi.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ambapo kila timu iliingia uwanjani hapo ikitaka kuibuka na ushindi ili kuweza kuchukua ubingwa wa michuano hiyo ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko zilitoka sare tasa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliingia ikiwa na hari kubwa kutokana na kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake ili kuweza kujiimarisha kwa lengo la kufanya vizuri katika michuano hiyo.
Wakionekana kucheza kwa umahiri mkubwa Kimoni FC walianza kwa kulishambulia lango la wapinzani wao bila kuwepo kwa mafanikio yoyote ambapo kila wachezaji walipokuwa wakipiga mashuti langoni mwao liligonga mwamba na kutoka nje.
Kutokana na ushindani wa mchezo huo ulizilazimu timu zote kutoka uwanjani dakika 90 bila kuona milango ya kila mmoja na hivyo mwamuzi wa mchezo huo kulazimika kupelekea mchezo huo kwenye mikwaju ya penati ambao ndipo kiomoni waliposhinda mabao hayo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mcheo huo wa Fainali Waziri wa Michezo,Sanaa na Utamaduni aliwapongeza waandaaji wa mashindano hayo huku akieleza kwamba mashindano ikiwemo Mbunge Ummy Mwalimu.
“Ukiona vyaelea ujue vimeundwa hili ya leo tuna kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Mbunge wetu Ummy Mwalimu niseme kama Waziri mwenye thamana ya michezo nimeshahudhuia mashindano yanayoandaliwa na wabunge mwengi sana sijaona mashindano mazuri kama haya”Alisema
Alisema mashindano haya ni mazuri na makubwa ambayo sijapata kuyaona katika maeneo mengine na Mbunge Ummy ana sifa ya kipekee kwa kuwajali wananchi wa Jimbo lake kutokana na kuhakikisha anawapigania ili kuweza kuondoa kero zenu.
Aidha alisema wanaposema michezo ni ajira wanaamini pia ni uchumi na wao kama Wizara wamemua hivi sasa michezo ni ajira na uchumi hivyo mashindano kama hayo watashirikiana na waandaaji kuhakikisha wanaibua vipaji na kuviendeleza.
Hata hivyo alisema kwamba mkoa wa Tanga ndio chimbuka la vipaji na wao serikali wataendelea kuiangalia Tanga huku akieleza kwamba Mbunge Ummy amepeleka ombi kwao kwamba uwanja huo wa Lamore ambao umechezewa fainali hiyo upandwe nyasi uwe mzuri ili fainali za mwakani ziwe nzuri .
“Na mimi nimemuhaidi Mbunge Ummy kwamba nitawaleta wataalamu kufanya tathimini ili uwanja uweze kuwa katikaa hali nzuri kutokana na kwamba umuhimu wa mashindano hayo ya Odo Ummy Cup”Alisema
Awali akizungumza katika fainali hiyo ,Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya alisema kwamba suala la Odo Ummy Cup ni mchango wake katika kutekeleza ilani ya CCM ibara ya 243 ambayo inawataka kuwekeza kwenye mpira wa migu hasa kwa vijana.
Alisema wanamshukuru pia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajab Abdurhaman kutokana na kwamba amekuwa akiwasaidia na kuwaleta na kuwaongoza kwenye kutekeleza ilani.
Aidha alisema mashindano hayo lengo ni kuwaleta pamoja vijana wa Tanga mjini na yameleta moja,mshikamano na hamasa ya kumweka karibu na vijana huku akishukuru timu zote kutoka Kata 27 ambazo zilishiriki kwenye michuano hiyo.
“Lakini pia nishukuru kamati za Siasa za CCM kwa kujitoa kusimamia mashindano hayo pamoja na timu ya Hamasa ya UVCCM pia niwashukuru wadhamini wetu kwa kuuunga mkono wakiwemo wadau wetu Assemble Insurance kwa kutuunga mkono”Alisema
Hata hivyo kwa upande wake,Mwenyeiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajab Abdurhaman atumia fursa hiyo kuwataka wabunge na madiwani wa mkoa huo wahakikisha wanaendelea michezo katika maeneo yao.
“Kwani kufanya hivyo ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ambayo tumehaidi kuendeleza michezo hivyo lililofanyika linatafsiri ilani kwa vitendo hivyo wabunge na madiwani hakikisheni hili linatekelezwa”Alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: