Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) , Bw. Griffin Mwakapeje akizungumza wakati wa Kikao cha Menejimenti ya Taasisi hiyo kilichofanyika leo Julai 6, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KATIBU Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) , Bw. Griffin Mwakapeje amesema Tume ipo kwenye mchakato wa kutekeleza Mpango wa kushirikisha vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini katika mashindano ya Uandishi wa Insha za masuala mbalimbali ya Kisheria na yenye changamoto katika jamii ili waweze kushiriki na kuchangia katika utaratibu wa marekebisho ya sheria kwenye maeneo husika.

Maelezo hayo ameyatoa wakati wa Kikao Cha menejimenti ya Taasisi hiyo kilichofanyika leo Katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Tume hiyo ambapo ameeleza kwamba yapo matukio mbalimbali yanayoibuka Katika jamii yenye mueonekano wa kisheria ambapo zikiandikwa Insha zinaweza kuisaidia Tume kupata taarifa za kitafiti.

Amesema kazi hiyo ya Uandishi wa Insha kwa wanafunzi itasaidia kuwajengea wanafunzi hari ya kufanya utafiti na kuiwezesha Tume kupata taarifa mbalimbali zitakazofanyiwa kazi Kwa kina na wataalamuwa Taasisi hiyo, Jambo ambalo litaongeza ufanisi wa Tume na maboresho ya sheria.

Aidha ameeleza kwamba washindi wa Insha watapatiwa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, kuchapishwa kwa maandiko yao kwenye jarida la tume, pamoja na vyeti na kwamba zoezi hilo litaongeza hamasa kwa wanafunzi kuwa wazalendo Katika nchi yao.

"Tutafanya makubaliano na vyuo mbambali hapa nchini kuhusu Uandishi wa Insha ili kuwa na uratibu mzuri wa zoezi hili ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi kufanya utafiti wa masuala mbalimbali ya kisheria yanayogusa jamii ili mwisho wa siku maandiko hayo yasaidie kufanya maboresho ya Sheria husika.

Katika kikao hicho, Bw. Mwakapeje amewahimiza wataalam na watumishi kuongeza jitahada kwenye utekelezaji wa majukumu na kuwataka wawe wabunifu ili kuyafikia malengo yao.
Kikao hicho kikiendelea.
Kikao kikifanyika.
Washiriki wakifuatilia kikao hicho.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akichangia jambo.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: