Watumishi wa Kada ya Udereva wa Bohari ya Dawa (MSD) kutoka Makao Makuu na Kanda zote 10 wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo yalioandaliwa na MSD yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
WATUMISHI wa Kada ya Udereva wa Bohari ya Dawa (MSD) wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo
iliwaweze kutoa huduma bora kwa wateja wakati wa usambazi wa bidhaa za afya.
Mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Morogoro yamewahusisha madereva wote wa
MSD kutoka Makao Makuu na Kanda zote 10 ambazo ni Dodoma, Mtwara, Kilimanjaro,
Kagera, Dar es Salaam, Iringa, Tanga, Tabora, Mbeya na Mwanza.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Rasilimali Watu , Adolar Duwe, amesema
kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa Wataalamu wa usambazaji bidhaa za
afya kwani yatawawezesha kuongeza uelewa juu ya huduma kwa wateja na namna ya
kuhudumia wateja wa MSD.
Akizumgumza kwa niaba ya Maderava wa MSD Bw. Erick Kaaya, amesema mafunzo
hayo yamewaongezea ujuzi, kujiamini na uelewa wa masuala mbalimbali ya muhimu
katika kuhudumia wateja.
Aidha ameiomba Menejimenti ya MSD, kuratibu mafunzo hayo mara kwa mara, ili kuwajengea uwezo na kuongeza tija katika utekelezaji wa shughuli za taasisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: