Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Simon Simalenga @official_simalengatz amefungua Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Vikundi 56 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ikiwa ni maandalizi ya kutoa mikopo ya Asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halimashauri ya Mji wa Bariadi kwa kuwahakikishia washiriki wa Mafunzo hayo kuwa Serikali Wilayani humo kupitia Halimashauri zake za Bariadi Mji na Halimashauri ya Wilaya ya Bariadi kuwa imejipanga kutoa mikopo zaidi kwa makundi hayo ikiwa ni utelekezaji maagizo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Simalenga amesema hayo mapema leo Februari 16,2023 alipokuwa anafungua Mafunzo ya Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Sekondari ya Bariadi Wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu lengo likiwa ni kuwaandaa wanafuika wa mikopo ili ikatumike kwa usahihi na kurudisha mikopo hiyo kwa wakati na hivyo kuwanufaisha watu wengi zaidi.

Kwa mujibu wa Simalenga mpaka sasa Halimashauri ya Mji wa Bariadi pekee imeshatoa mikopo kwa wanufaika 2,655 ambao wamepokea mikopo ya jumla ya shilingi 1, 054,284,000 ambapo katika makusanyo ya Julai mpaka Disemba 2022 Serikali Halimashauri itatoa mikopo ya shilingi 244,170,000 ikiwa ni asilimia 10 ya makusanyo kwa kipindi hicho

Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka washiriki wa Mafunzo kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika urejeshaji wa mikopo hiyo na kuondokana na dhana kwamba fedha hizo ni za bure kwasababu kwa kutokuzirejesha kunawanyima fursa ya mikopo Watu wengi zaidi.

“Ndugu Wanavikundi niwape angalizo kwamba kila atakaepata mkopo ahakikishe anarudisha mkopo husika kwa wakati kwasababu sheria iliyotoa maelekezo ya kutoa mikopo kwenu pia imeweka utaratibu wa hatua za kuchukua kwa wasiorudisha Fedha hizo. Mpaka sasa kiasi cha shilingi 185,977,000 bado hakijarudishwa kutoka kwa wanufaika wasiokuwa waaminifu, hili halitavumiliwa hata kidogo”. Simalenga aliasa

Ibara ya 24(b) katika ukusara wa 20 wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha MAPINDUZI ya mwaka 2020/2025 Chama hicho kimeielekeza Serikali kutoa asilimia 10 ya makusanyo kwa kila halimashauri hapa nchini na kutoa mikopo kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ili kujikwamua kiuchumi.


Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: